Hivi majuzi mwanadada Huddah Monroe wa Kenya alitoa
kauli kwenye mtandao kwa mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond platnumz
juu ya Wema Sepetu kwa kumwambia kuwa “asihangaike na wadada wengine
kwani wema ndio kipenzi chake na hao wengine wote ni wapiti njia” kauli
ambayo kwa muda mfupi tuu imemfanya mwanadada huyo awe gumzo la mitandao
hapa nchini na “kuchafua hali ya hewa” huko kwenye mitandao mbalimbali
ya kijamii na isiyo ya kijamii kwa watu wanopenda na wasipoenda penzi la
wawili hawa
Uchunguzi uliofanya na bongomovies umebaini kuwa mashabiki wengi
wa muziki na filamu hapa nchini wanapenda sana mahusiano baina ya wawil
hawa (Wema na Diamond) kiasi cha kusababisha kuanzishwa kwa makundi
mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii yakichochea wawili hawa kuoana na
ikiwezekana kuzaa watoto haraka iwezekanavyo.
Katika pitapita zetu kwenye mtandao tuliweza kupata kauli hizi
za watu mbalimbali wakimsifia Huddah kwa kauli yake hiyo huku wengine
wakimuona kama ni shujaa….
“Umenifurahisha sana leo yaan had nime comment!!@huddahmonroe”
mmoja wapo aliandika…
“Kuanzia leo nakupenda bureee….na nakufollow@huddahmonroe”
mwingine aliongezea…
“Nakupenda bureee Huddah we ni shujaa”… mwingine naye aliongezea huku wakidiriki kusema kuwa wawili hawa wakioana basi itakuwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa kwao.
Bongo Kazi kweli kweli!