![](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/11/dimonddd.jpg?width=552)
MKALI wa wakali kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amezidi
kutanua wigo wa muziki wake baada ya kutua pande za Nigeria na kufanya
video mbili na wakali wa pande hizo, Dvido na Iyanya.
Diamond alifanya wimbo wa Number One Remix na Davido alipokanyaga
ardhi ya Tanzania katika Tamasha la Fiesta, wakati huohuo alifanikiwa
kufanya wimbo mwingine na Iyanya ambaye pia alikuja kutumbuiza katika
tamasha hilo.
“Huwa nazitumia fursa kila zinapotokea, watu wengi hawakujua kama wasanii hao walipokuja nilirekodi nao ngoma mbili
tofauti.
“Ilikuwa tufanye na video kabisa hapa Bongo lakini kutokana na tatizo
la kiufundi lililotokea katika Viwanja vya Leaders, wasanii
hao walilazimika kufanya shoo siku ya pili yake vivyo kuharibu kabisa ratiba nzima,” alisema Diamond.
Kuhusu video hizo, Diamond aliweka plain kuwa atahakikisha kuwa zinakuwa bora zaidi ya ile ya Number One ambayo
aliifanyia Afrika Kusini hivyo kuwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula.
“Lengo langu ni kujenga ukaribu na wasanii wa Nigeria, ni fursa moja wapo ya kuusogeza muziki wetu katika levo za
kimataifa,” alisema Diamond.
Mkali huyo anatajwa kuwa gumzo katika kolabo za wasanii wa kimataifa kumzidi hata Ali Kiba ambaye aliwahi kufanya kolabo
na wasanii wengi wa nje katika wimbo wa One 8 ulioandaliwa na R-Kelly kutoka pande za Marekani lakini kwa sasa amefifia.
source ;GPL