Safari ya fundi fataki kwenda jela mwaka mmoja ikianzia hapa
………………………………………………………….
FUNDI magari mkazi
wa kijiweni katika Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Bw Abdul Husein (31)
amejikuta akitupwa jela
mwaka mmoja na faini ya shilingi 200,000 baada kutiwa
hatiani na mahakama ya mwanzo bomani kwa
kosa la kutaka penzi la nguvu kwa
mwanafunzi wa darasa la tano .
Fundi huyo
ambaye anadaiwa kukaribishwa katika nyumba
hiyo kama mlinzi wa watoto
wawili akiwemo mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa hilotarehe 4 mwezi huu majira ya saa
3 usiku baada ya
kurejea kutoka katika shughuli
zake.
Akisoma hukumu hiyo
leo hakimu mkazi
wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua alisema
kuwa katika ushahidi
ambao ulitolewa mahakamani hapo na mtoto
wa kiume wa miaka 9 ulidai kuwa kijana
huyo siku ya tukio baada ya kufika
nyumbani alimtaka binti huyo
kumpa sahani ili
aweke chips ambazo alikuja
nazo .
Kuwa baada ya binti
huyo jina limehifadhiwa na mtandao huu kumpa
sahani ndani ya dakika chache
aliomba kupewa maji na binti
huyo alifanya hivyo baada ya
kupewa maji kijana huyo alimtaka binti huyo
kusogea kukaa katika
eneo kochi ambalo fundi huyo amekuwa akilitumia kama kitanda
chake sebuleni kama mlizi bado binti
huyo aligoma kuingia majaribuni .
Hata hivyo haikuishia hapo baada ya
muda fundi huyo fataki
alimtaka binti huyo kumsindikiza chooni bado binti
alionyesha msimamo wa kutamani
masomo yake na kugoma
kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni binti
na huyo ni mwanaume iweje aombe kusindikizwa .
Kutokana na mbinu
zote kugonga mwamba
ndipo fundi fataki
huyo alipoamua kutumia njia ya
mkato ya
kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka kumbaka
chooni kabla ya binti huyo kuamua
kupambana na kuishia kuchaniwa sketi yake .
Hali hiyo ilimfanya
binti huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama yake aliyekuwa amelala chumba cha
pili kabla ya mama mzazi na
majirani kuamka na kumwadabisha
fundi fataki kwa kumpeleka polisi.
Hakimu Masua alisema
kuwa kutokana na ushahidi
uliotolewa fundi huyo
alipotakiwa kujitetea alikana
kujitetea kwa madai kuwa hawezi
kuzungumza chochote katika mahakama
hiyo.
Hivyo alisema kutokana
na mtuhumiwa huyo
kutenda kosa hilo kwa mara ya
kwanza mahakama hiyo ilipaswa
kumfunga jela kwa miaka mitano
kutokana na kosa hilo la shambulio la aibu kifungu
cha 135 kanuni ya adhabu namba 6
marejeo mwaka 2002 .
“ Mahakama hii inakuona na
hatia na hivyo
inakupunguzia adhabu kutoka miaka
mitano uliopaswa kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela na
ukitoka utatakiwa kumlipa
mlalamikaji kiasi cha Tsh 200,000”
chanzo;franciss godwin
|