Gumzo kubwa kwenye harusi
ya staa wa dunia katika Kundi la P-Square wanaotarajiwa kuangusha shoo
Bongo kesho, Peter Okoye mwishoni mwa wiki iliyopita, ni mwaliko wa
msanii pekee wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alipondwa
kwa kuvaa suruali ‘njiwa’ (ya ajabuajabu).
Ishu hiyo ilijiri huko Lagos, Nigeria ilikofanyikia sherehe hiyo
ambapo Peter alifunga ndoa ya kimila na mrembo wa haja, Lola Omotayo
huku Diamond akipata fursa ya kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa
duniani, kasoro pekee ikawa kwenye mavazi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Diamond alichemka
kwa kuvaa kivazi hicho kifupi miguuni kikiwa na mistari myeupe na myeusi
hivyo kusababisha kutukanwa mitandaoni.
WEMA, JOKATE KIVIPI?
Huku wakitumia picha za waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond, Wema Isaac
Sepetu na Jokate Mwegelo wakiwa wamevaa ‘taiti’ kama ‘kisuruali’ cha
mwanamuziki huyo, walieleza kuwa inawezekana wao ndiyo walimdizainia
hivyo kumsababishia matusi ya nguoni katika mitandao ya kijamii.
“Mafashenista wengi wanamtukana Diamond lakini inawezekana na zile
nguo kadizainiwa na Wema au Jokate kwa sababu ni staili zao. Nao wana
nguo kama hizo, hebu cheki kwenye picha,” alisema mmoja wa wachangiaji
wa mada hiyo katika mitandao ya Naija huku akitundika picha za Wema na
Jokate wakiwa wamevaa kama Diamond.
“Ni kweli Diamond amepata nafasi
kubwa ya kukutana na mastaa wakubwa na kutangaza muziki wake kimataifa
lakini kitu kimoja hakikwenda sawa.
“Ni juu ya nguo aliyokuwa ameivaa, mashabiki wengi wa muziki nchini
Nigeria walisema kachemka,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni ya
mashabiki wa muziki nchini humo.
Hata staa wa Nigeria aliyekuwa
mmoja wa wenyeji wa Diamond, Iyanya alipoposti picha akiwa na Diamond
pamoja na jamaa mwingine, ‘polisi jamii’ wa masuala ya mitindo
waliendelea kugongea msumari wa moto kuwa Diamond akubali kuwa kachemka.
STAILI YA MICHAEL JACKSON?
“Iyanya, nani huyo kavaa suruali kama (marehemu) Michael Jackson? Mungu
nisamehe kwa kukutenda dhambi lakini ukweli hicho kivazi hakiendani na
mwili wake,” alifunguka shabiki mwingine kwenye ukurasa wa Iyanya wa
Instagram.
Mwingine alisema: “Najua amekopi kwa mtu wake
anayemhusudu (Wema), alionekana amependeza alipovaa hivyo walipokuwa
China. Ukweli (Diamond) hakupendeza au labda kachukulia kwa Jokate wa
Kidoti?”
ANGEENDA KUBADILISHA
Baadhi ya
mashabiki hao walidai kuwa Diamond alipaswa kugundua kuwa yupo tofauti
na mastaa wengine ili arudi hotelini mara moja akabadilishe nguo.
“Sijui alifikiria nini alipovaa hivyo, ona sasa amewaangusha na kuwadhalilisha mastaa wa Tanzania huko Afrika Magharibi.
“Ukweli ni kwamba kama alimuiga Wema na Jokate kachemsha, ona sasa wamemponza kwa kuvaa njiwa ya zebra kama wao.
“Diamond anajua kuvaa sana lakini anapaswa kuwa na dizaina wa kumpa
ushauri wa mavazi kabla ya kwenda kwenye shughuli kubwa kama ile,”
aliandika Mtanzania aishie Nigeria.
KAPATA ‘KIKI’?
Katika kujitetea huku akiamini kapata ‘kiki’ nchini Nigeria, Diamond
alitumia ukurasa wake wa Instagram kwa kutundika picha yake akiwa na
kisuruali hicho akiambatanisha na mastaa wakubwa wa Marekani kama akina
Wiz Khalifa wakiwa wamevaa njiwa kama yeye kuonesha kuwa ni fasheni ya
‘mbele’.
Hata hivyo, hiyo haikusaidia kwani mashabiki hao
waliendelea kumponda na kumtaka kujipanga zaidi siku akipata fursa kama
hiyo kwani mastaa aliojifananisha nao walivaa hivyo katika ‘iventi’
tofauti na harusi.
MAMODO WANASEMAJE?
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya mamodo maarufu wa Kibongo ambao walishuhudia vazi hilo ambapo walikuwa na haya ya kusema:
“Sijui ni nani aliyemdizainia lakini kilichofanyika ni kwamba
alimvalisha Kimarekani, akasahau kuwa alitakiwa amvalishe Kiafrika au
Kitanzania. Unajua harusi yenyewe ilikuwa ya kimila haikutaka Umarekani
hata kidogo ndiyo maana watu walimponda Diamond. Naamini wakati mwingie
aliyemvalisha atafanya vizuri,” alisema modo maarufu wa Kiume Bongo,
Martin Kadinda.
“Unajua mitindo ya mavazi unaweza ukatulia,
ukadizaini kitu lakini ukifika mbele za watu wakakushangaa, hiyo ndiyo
fasheni ilivyo. Simlaumu Diamond wala sisemi alitakiwa ashone khanga au
kitenge lakini iwe changamoto kwa mamodo wetu waongeze ubunifu,” alisema
modo mwingine.
Pamoja na mambo mengine, safari ya Diamond nchini
humo ililenga kwenda kufanya kolabo na mastaa wawili wa Nigeria, Davido
na Iyanya.
CHANZO;GPL