Stori: IMELDA MTEMA
UTATA umeibuka kufuatia
kuwepo kwa taarifa kuwa huenda modo maarufu aliyedaiwa kushikiliwa nyuma
ya ndondo kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, Jacqueline
Patrick ameachiwa huru.
Utata huo uliibuka mapema wiki hii mara baada ya akaunti ya modo huyo
katika mtandao wa Instagram, kuposti picha mpya za Jack hali
iliyowafanya wafusi wa mtandao huo kuamini kwamba yupo huru.
“Haiwezekani mtu awe lupango halafu aweze kuingia Instagram na kuweka
picha mpya…au kaachiwa huru?” ilihoji mmoja wa wadau wa mtandao huo.
Baada ya komenti hiyo, wafusi wengi mtandaoni waliweza kuamini kuwa
aliyeposti picha hizo ni Jack kwani akaunti iliyotumika ni ileile
aliyokuwa akitumia modo huyo.
Paparazi wetu naye hakuwa nyuma, alijiridhisha kwa kutazama baadhi ya
komenti za kipindi cha nyuma ambazo aliwahi kukomenti katika picha za
modo huyo na kuamini kabisa akaunti iliyoposti picha mpya ni Jack.
Wakati tunakwenda mitamboni, mdau mmoja wa burudani alihojiwa na
kusema huenda akaunti hiyo ya Jack imetumiwa na msanii wa Bongo Fleva
anayefahamika kwa jina la Jux ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wake,
alipoulizwa Jux, alisema:
“Jack yupo fresh kabisa niliongea naye…ila amesafiri…”
Jack alidaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kilo 1.1
Desemba 19, mwaka jana. Hadi leo sakata lake linawafanya watu wabaki
gizani wasijue kinachoendelea.
CHANZO>GPL