Na Waandishi Wetu
AMA kweli maovu yanazidi kuongezeka, shetani naye mbioni siku zote
kunasa waliyo wake, kauli hizo zote ziko sambamba na staa wa sinema za
Kibongo na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Joseph Madaha amenaswa
baada kuingia mkenge mtego wa kujiuza, Ijumaa limesheheni.
Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo hujihusisha na
biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na kufanya sanaa kuwa kama
chambo cha kunasa wanaume.
OFM MZIGONI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini
ya Global Publishers, mwaka jana ilinasa mastaa wawili kwenye mtego
wake, mke wa mtu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na Lulu Mathias
Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Mwaka huu, OFM imeanza kazi zake ambapo kwa kuanzia iliamua kumtega Baby Madaha aliyejaa kwenye kumi na nane zake.
Mmoja wa wadau wa OFM alijifanya mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye
ni mgeni wa jiji a.k.a Ngosha akijipachika jina la Frank ambapo baadaye
katika mazungumzo, Baby Madaha alimbana na kutaka ampatie majina matatu
ndipo mwana-OFM Frank (feki) akajipatia jina Frank Michael Lugwisha.
ILIKUWAJE?
Mchezo mzima ulianza Januari 13, mwaka majira ya saa 11:52 jioni kwa
kuchati kwenye simu ya kiganjani ambapo Baby Madaha aliingia
kichwakichwa bila kujua anachati na ‘sumu’ wa OFM kama ifuatavyo;
Frank/OFM: Mambo vipi Baby Madaha? Nilikuwa naomba tuonane.
Baby Madaha: Kuhusu nini?
Frank/OFM: Niwe mkweli, Madaha nimekupenda, nilipofika hapa Dar ndo nikaona nikutafute.
Baby Madaha: Unampendaje mtu usiyemjua?
Frank/OFM: Jamani nakuonaga magazetini na video zako.
Baby Madaha: Safi, so unataka kuniambia nini ambacho sijakisikia?
Frank/OFM: Nataka tu-meet (kukutana) Madaha nimetokea kukupenda sana lakini Alhamisi (jana) narudi mkoani Mwanza.
Baby Madaha: Huwezi ku-manage kuwa na mimi, baki kuwa shabiki wangu tu.
Frank/OFM: N’take radhi Madaha, kwa nini nisiweze, kikubwa kipi?
Baby Madaha: Huh! Tuma vocha tuone how worth are you? (Tuma vocha tuone utajiri wako)
Frank/OFM: Acha utani bwana, vocha kitu gani, ongea mambo makubwa Madaha
Baby Madaha: Hahaha…yote ninayo-except vocha tajiri.
Frank/OFM: Acha bwana. Vocha ndo kikwazo kwako?
Baby Madaha: Yap! Kama hutaki acha au unadhani natumia wireless kuchati na wewe?
Frank/OFM: Madaha wewe ni mkatili kiasi hicho?
MAMBO YASIMAMA KWA MUDA
Masuala ya kuchati
yalisimama kwa muda lakini ilipofika saa 2:22 usiku, mazungumzo
yaliendelea ambapo siku iliyofuata Frank wa OFM aliamua kuendelea
kumtengenezea mtego ili kujiridhisha kama ni kweli baadhi ya mastaa wa
Bongo wanafanya biashara hiyo haramu.
Januari 14, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi, Frank wa OFM alianza tena kuchati na Baby Madaha kama ifuatavyo;
Frank/OFM: Mambo Madaha? Mi Frank
(akaamua kumpigia simu Frank wa
OFM, ilikuwa mshtuko kwa Frank kwa sababu hakujipanga kuongea naye kwa
hiyo hakupokea simu ya Baby Madaha ambayo ilipigwa saa 6: 30 mchana.
Dakika moja baadaye, Baby Madaha alituma meseji ya kumtoa hofu Frank wa OFM;
Baby Madaha: Frank ‘am calling you in vain uh afraiding of me (Frank nakupigia kwa nia njema unaniogopa?)
Frank/OFM: Sorry nilikuwa tight, naweza kupiga?
Baby Madaha: Yap!
Frank/OFM: Frank wa OFM aliongea na Baby Madaha na kuanza kumchomekea
ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kuonesha nia ya kujenga uhusiano
huku akimtaka staa huyo kuwa ‘siriaz’ akimuahidi kuwa atakuwa naye na
kuwa ajenti wake wa muvi jijini Mwanza.
Baada ya maongezi ya kutongozana kwenye simu, Frank wa OFM alimtumia tena meseji Baby Madaha kama ifuatavyo;
Frank/OFM: Nimefurahi sana kuongea nawe, sijui itakuwaje tukionana?
Baby Madaha: Wait, you I’ll see.
Frank/OFM: Eti ee, nimetokea kukupenda sana.
Baby Madaha: Thanks.
Baada ya hapo Frank wa OFM alimaliza kumtumia ‘sms’ siku hiyo, ilikuwa saa 9:12 alasiri.
Hata hivyo, Frank wa OFM aliamua kumhoji zaidi kupitia sms akitaka
kujua hasa akiwa naye hata kwa saa tatu atataka shilingi ngapi?
Frank/OFM: Sasa hivi nataka kutoka niende ATM kuchukua pesa, sasa hebu
kuwa muwazi tu wangu, kuwa na wewe kwa kama saa tatu utakuwa poa nikupe
Sh. ngapi? Mtu mzima nisije nikaumbuka si unajua tena kwa staa kama
wewe?
Baby Madaha: Milioni 10!
Frank/OFM: Baby usinikomoe, mimi na wewe tuna safari ndefu, kila nikija Dar tutakuwa pamoja.
Baby Madaha: (…anapiga simu lakini Frank wa OFM hapokei).
Baada ya kuona hivyo, Baby Madaha alituma sms hii “Call” (piga).
MAONGEZI YA SIMU
Frank/OFM: Mambo vipi Baby, habari za muda tena?
Baby Madaha: Salama tu, kwani wewe ulikuwa unataka kutoa sh. ngapi ATM?
Frank/OFM: Mimi ndiyo nilikuwa njiani naelekea ATM natoka hapa hotelini
nilipofikia nina Shilingi Mil.4 kwa usiku mmoja, hapo vipi?
Baby
Madaha: Katoe 5 fresh, sasa benki gani utaenda kutoa wakati benki zote
zimeshafungwa na ATM mwisho kutoa ni Mil.1, sasa hapo itakuwaje?
Frank/OFM: Nitatoa kwa ATM, hata hivyo, nina master-card, naweza
kutoa Mil.1 hadi mara 5, usijali kwani pesa kitu gani, cha msingi mimi
ni kuwa na wewe!
Baby Madaha: Okay, fine unaweza kuja Kijitonyama (Dar) hapa kwenye hoteli ya (anaitaja jina)?
Frank/OFM: Nimefikia hapa hotelini (jina kapuni), sasa kutoka ni vigumu.
Baby Madaha: Okay, poa nitakuja hapo hotelini saa 1:00 usiku.
Frank/OFM: Usijali karibu sana, nakupenda sana Baby Madaha yaani niko tayari kwa lolote, sema unataka nikupe nini?
Baby Madaha: Hahaha….(anachekaaa) nikija nitakwambia vyote ninavyotaka kwani unafanya biashara gani?
Frank/OFM:
Nauza nguo, mara nyingi nafuata Jakarta, Indonesia mara kwa mara lakini
natumia muda mwingi kufanya kazi zangu Mwanza.
Baby Madaha: Wee Msukuma eti? Mimi mwenyewe Msukuma kwani unadhani jina Madaha ni la nini hilo, mimi mwenyewe Msukuma.
Frank/OFM: Nimefurahi sana kusikia hivyo, unaweza kuongea Kisukuma?
Baby Madaha: Naweza, wewe nisemeshe tu!
Frank/OFM: Nakutogilwe gete Madaha (Frank anaongea Kisukuma kwamba anampenda sana Madaha)
Baby Madaha: Tukuhoya ntondo nduhu tabu (anajibu kwa Kisukuma kuwa hakuna tatizo tutaongea kesho).
Ulipofika muda waliokubaliana na Frank wa OFM, Madaha alisema kuna
foleni kubwa hivyo kuna sababu ya kubadilisha hoteli hiyo iliyoko maeneo
ya Ubungo alipopanga Frank wa OFM waonane, Baby Madaha akataka wakutane
nyingine iliyoko Kijitonyama.
“Siwezi kuja huko, kwanza kuna
mifoleni isitoshe ni vizuri ukafika mwenyewe maeneo haya ya hoteli ya…
(anataja), ni sehemu nzuri kwangu hivyo kama huna nia mbaya na mimi ni
vizuri ukaja maana kesho nasafiri kwenda Kenya kwenye shughuli zangu za
muvi, kwa hiyo unaweza kuja wewe tu maeneo haya,” alisema Madaha.
Frank
aliendelea kumbana kwamba tayari alikuwa ameshaandaa pesa shilingi
Mil.5, kama walivyokubaliana lakini asingeweza kubeba mfuko wa fedha
wote huo isitoshe ni hoteli ambayo ameizoea kwa muda mrefu.
“Ujue
Dar mimi siyo mzoefu, achilia mbali kuogopa kutapeliwa hivyo nakuomba
uje kwenye hii hoteli nitafurahi sana dear, nakuomba unielewe ujue
nakupenda sana mpenzi wangu Baby Madaha, tulia tuyajenge maisha,”
alisema Frank wa OFM.
Msanii huyo alimkomalia Frank wa OFM wakutane siku ya Jumanne usiku
ambapo alimwambia pia kuwa amepata dharura anakwenda kumuona
mfanyabiashara mwenzake kwenye hoteli moja iliyopo Masaki (jina tunalo)
ambapo Baby Madaha alitaka waonane na Frank wa OFM kwenye hoteli
hiyohiyo.
“Nimepata dharura sitaweza kuonana na wewe, naenda kumuona
mfanyabiashara mwenzangu maeneo ya hoteli…(jina tunalo), tuonane kesho
muda wa asubuhi,” alisema Frank.
Baadaye Frank alimjulisha mteja wake kuwa yuko njiani anafuata mzigo
bandarini akitoka wataonana na Baby Madaha kesho yake asubuhi ya
Jumatano iliyopita, alituma sms hii;
Baby Madaha: Kuna stage tano
in anything, nakupa tatu, coz uko siku ya tatu, denying, bargaining,
accepting….. tomorrow if you be still on game, i give you the remained
good day, enjoy Mr Frank, ukitoka cargo call me, we meet!
Frank/OFM: Okay, siku njema nitakutafuta.
Baby
Madaha: Matajiri wengine hawana maneno kama wewe kwa mfano…(anataja
jina la pedeshee mmoja maarufu Dar). Wanatuma pesa na siyo maneno, wee
tuma hela (-)-pesa ipo kila sehemu we tuma ndo nitaweza kujiongeza kama
nakuja au laa.
Frank/OFM: Nakutumia muda siyo mrefu, usijali.
IJUMAA LAMBANA BABY MADAHA
Hata hivyo, Baby
Madaha hakutumiwa pesa alizotaka ili kukamilisha zoezi badala yake, OFM
walitua mzigo wa ushahidi kwenye dawati la Ijumaa ambalo lilikuwa na
jukumu la kutafuta mzani wa ishu hiyo.
Ijumaa lilipomtafuta Baby
Madaha alikiri kuwa kwenye mawasiliano na mwanaume aliyemtaja kwa jina
la Frank Michael Lugisha ambaye alisema alikuwa akifanya naye
makubaliano ya kusambaza filamu yake ya The Gal Bladder.
Alipobanwa juu ya makubaliano ya kujiuza kwa mwanaume huyo kwa Sh.
milioni 5 alikataa pamoja na kwamba alielezwa kuwa kuna ushahidi wa
meseji na sauti.
Alipotakiwa kufika kwenye ofisi za gazeti hili ili
kusikilizishwa sauti na kuoneshwa meseji zake, Baby Madaha alisema
hawezi kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda nchini Kenya muda mfupi
baadaye.
CREDITS,,,GLOBAL PUBLISHERS