Mashabiki wa Simba |
Matokeo ya mchezo la ligi kuu ya
Voda Com si Simba wala Mbeya City baada ya timu hizo zote mbili
kutoka uwanjani hapo kwa kifua mbele cha goli 1-1.
Mchezo huo ambao kwa Mbeya City ni
mchezo wa nyumbani imeweza kuonyesha umakini mkubwa wa kugomea
kufungwa katika uwanja wa Nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya huku
Simba nayo ikikwepa ” kugagaduliwa ” ugenini kiasi cha kuifanya Simba
kukomaa na kusawazisha goli la Mbeya City lililofungwa kipindi cha
kwanza huku Simba ikisawazisha goli hilo kipindi cha pili .
Timu ya Mbeya City ambayo awali
iliweza kufanya vema kwa Yanga kulazimisha sare pia leo imeweza
kulazimishwa na Simba kutoa sare ya goli 1-1
Wakati huo huo timu ya Lipuli Fc
Iringa imefanikiwa kuichapa timu ya Polisi Morogoro katika mchezo wa
ligi daraja la kwanza mzunguko wa pili kwa jumla ya goli 3-1
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Samora mjini Iringa huku wadau wa soko wakiipongeza kwa mchezo huo.