baada ya kuilaza Arsenal mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates mjini
London usiku huu katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Bao hilo pekee lililoizamisha Arsenal
iliyomaliza pungufu ya mchezaji mmoja, lilipatikana dakika ya 54,
mfungaji Toni Kroos aliyefumua shuti kali akiwa umbali wa mita 20 baada
ya pasi ya Philipp Lahm.
Thomas Muller akafunga bao la pili dakika ya 88 baada ya pasi nzuri ya Philipp Lahm tena.
Arsenal ilipata pigo dakika ya 39
baada ya kipa wake Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa kadi nyekundu
kufuatia kumuangusha winga wa Bayern Munich, Arjen Robben kwenye eneo la
hatari.
David Alaba akaenda kupiga penalti,
lakini pamoja na kumpoteza maboya kipa Fabianksi akapiga nje mpira huo
pembeni mwa nguzo ya lango chini.
Mapema dakika ya nane, Arsenal
walipoteza nafasi nzuri ya kupata bao, kufuatia Jerome Boateng kumkwatua
hadi chini Mesut Ozil ndani ya boksi, lakini kiungo huyo Mjerumani
akaenda kupiga penalti mbovu kabisa ikapanguliwa kiulaini na kipa
Manuel.
wa akiba Lukasz Fabianksi aliingia
badala ya Cazorla akaenda kusimama langoni, na tangu hapo Arsenal
wakalazimika kucheza mchezo wa kujihami.
Katika mchezo mwingine usiku huu, bao
pekee la Diego Costa dakika ya 83 limeipa Atletico ushindi wa 1-0
ugenini ya wenyeji AC Milan Uwanja wa Giuseppe Meazza. Chanzo:
binzubeiry