mawili na kuisaidia Paris St-Germain kusajili ushindi mkubwa wa mabao
4-0 dhidi ya Bayer Leverkusen katika mchuano wa ligi ya mabingwa barani
Ulaya.
Blaise Matuidi ndiye aliyefungua mvua
hiyo ya mabao alipotikisa wavu kunako dakika ya tatu ya ya kipindi cha
kwanza na kumwacha kipa Bernd Leno amezubaa.
Ibrahimovic alifunga mkwaju wa adhabu na kuipa PSG bao la pili kunako dakika ya 39 .
Dakika tatu baadaye Ibrahimovic
alifunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti, Spahic alipomzuia
Ezequiel Lavezzi na refarii akaiadhibu Leverkusen.
Wafungaji bora Ligi ya Mabingwa 2013-14
Zlatan Ibrahimovic (PSG) 10
Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 9
Lionel Messi (Barcelona) 7
Sergio Aguero (Man City) 6
Alvaro Negredo (Man City) 5
Mechi hiyo ilibakia kuwa ya nipe
nikupe hadi muda wa lala salama ya kipindi cha pili hadi pale Yohan
Cabaye alipocheka na wavu punde baada ya Emir Spahic kuonyeshwa kadi
nyekundu kwa kucheza visivyo.
Kutokana na mabao hayo mawili
Ibrahimovic,sasa amempiku mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo kwenye
orodha ya mfungaji bora katika msimu huu wa mwaka 2013-2014 wa ligi
yenye kitita kikubwa zaidi barani ulaya akiwa na jumla ya mabao kumi.
Chanzo: bbcswahili