MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu
kama Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi
anayejulikana kwa jina moja la Nagar.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo
aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na
Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu
sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati
zake za kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa
albamu ya Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya
kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga
simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni
maneno ya watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,”
alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema
anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema
kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi,
ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema
bila kufafanua zaidi.
CREDIT: GPL