DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba
mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii
waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii
waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea
haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa
Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na
watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa
kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu
wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.