![Britney Spears’ Weird Tour Rider](http://www.hollyscoop.com/sites/hollyscoop.com/files/styles/block_photo_normal/public/p18bhc99vobdc3c12gp1plt19p74.jpg?itok=OqQAdzUt)
Britney Spears amekuwa katika hoteli ya Planet Hollywood Resort jijini Las Vegas katika tour yake ya Peace of me.
Diva huyo mkali wa muziki wa Pop ambaye amewahi kukimbiza na vibao vikali kama “Baby more time”, “Womanizer”, “Ooops! I Did It Again”, “I Am A Slave For You” na “Toxic” amekuwa gumzo katika jiji la Las Vegas hasa kwa ukali wa shoo zake katika hoteli hiyo ya Planet Hollywood.
Britney ana mkataba wa miaka miwili ya show katika hoteli hiyo kitu ambacho kimemfanya aishi jijini Las Vegas kuanzia Disemba mwaka jana na alitarajiwa kumaliza mkataba wake Septemba mwakani lakini gazeti la New York Daily News limeripoti kuwa kuna uwezekano wa kuongezewa mkataba kwani wamiliki wa hoteli hiyo wameridhishwa na maingizo ya shoo za Britney. Hivyo makazi ya Britney yataendelea kuwa Las Vegas