Kampeni zinazoendelea hivi sasa kote Ulimwenguni ni kampeni za kupinga vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na Boko Haram kwa kuwateka wanafunzi wa kike na kuwafanyia vitendo vya kigaidi huko nchini Nigeria. Kampeni hizo ambazo ni maarufu kama “Bring Back Our Girls” zimekuwa zikihamasihwa na mastaa tofauti kutoka kote Duniani lakini mwanamitindo Irina Shayk ambaye pia ni mpenzi wa mchezaji bora Duniani, Christiano Ronaldo ametumia semu ya kifua chake akiwa hajavaa nguo kabisa kuweka bango ambalo linasisitiza kurudishwa kwa wasichana hao waliotekwa na Boko Haram. Picha hiyo aliitupia katika mtandao wa instagram na kuibua hisia mbalimbali za wadau, huku wengi wakiponda kitendo cha Shayk kuacha kifua wazi kuwa hakiendani na mada hiyo anayoipigia kampeni.
Baadhi ya watu walioponda kitendo hicho waliandika maneno kama “Vaa nguo zako we mpuuzi usiyejiheshimu”
Mwingine aliponda kwa kusema “Huu ni upuuzi uliopitiliza, kushikilia hicho kipeperushi mbele ya matiti yako kama vipeperushi ambavyo huwa wanavaa mamiss vifuani mwao” Hivi kweli? HIYO HAIKUFAI.
Lakini wadau wengine walimsifia Irina Shayk kwa kutumia nafasi yake kukemea hali iliyopo Nigeria kwa sasa, na waliongeza kusema kwamba chochote kitakachokuwa kinaunga mkono kampeni za #BRING BACK OUR GIRLS kitathaminiwa.