Mmiliki wa klabu ya soka ya Uingereza Manchester United, Malcom Glazer amefariki jana Jumatano akiwa na umri wa miaka 85.
Glazer ambaye ni mfanyabiashara Mmarekani, pia alikuwa raisi wa klabu ya soka ya huko Marekani ijulikanayo kwa jina la Tampa Bay Buccaneers.
Malcom aliinunua Man U mwaka 2005 na Man U imeshinda vikombe vitano vya ligi kuu ya Uingereza, kimoja cha UEFA na kimoja cha klabu bingwa ya Dunia ikiwa chini ya uraisi wake.
Mashetani wekundu wameandika kwa masikitiko katika website yao “Fikra za kila mwana Manchester United ziko na familia ya Glazer katika kipindi hiki kigumu”
Marehemu ameacha mke mmoja Linda, watoto 6 na wajukuu 14.
HARAKATI 360 inaungana na familia ya wana Man U kuomboleza kifo hiki, Mungu amlaze pema.Amen