Kwa mara ya kwanza wasanii kutoka bara la Afrika wametajwa kutumbuiza katika sherehe za ugawaji wa tunzo za BET zitakazofanyika June 29 huko Los Angeles Marekani ndani ya ukumbi wa Nokia Theatre . Waandaaji wa tunzo hizo wamewataja Mafikizolo kutoka Afrika Kusini, kutoka Nigeria mwnadada Tiwa Savage na mkali Ice Prince wametajwa huku list hiyo ya watumbuizaji kutoka Afrika ikifungwa na mwanahiphop bora wa Afrika, Sarkodie kutoka Ghana.
Katika tunzo hizo Mtanzania Diamond Platnumz pamoja na Mnigeria Davido wanawania tunzo ya mwanamuziki bora wa kimataifa kutoka Afrika (Best International Act-Africa)
Wasanii wa Marekani watakaotumbuiza ni pamoja na Trey Songz, Lionely Richie, K Michelle, Mack Wilds, Jeniffer Hudson Mary J Blige na wengine kibao. Huku muongoza shughuli akiwa ni muigizaji maarufu kutoka nchini humo, Chris Rock.