Rapa wa nchini Marekani Radric Davis maarufu zaidi kama Gucci Mane amejikuta akionja joto ya jiwe baada ya hakimu Steve C. Jones kuamuru kifungo cha miaka mitatu na miezi mitatu kwa mwanamuziki huyo. Hukumu hii imetolewa baada ya rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 kukutwa na hatia ya kumiliki bastola kinyume cha sheria na kufanya vurugu mtaani baada ya kutumia bangi. Polisi walisema wao walipokea taarifa kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha kama rafiki wa Gucci Mane kuwa rapa huyo anafanya fujo mtaani, na walipofika Gucci alikuwa akinuka bangi na walipomkagua walimkuta na begi ambalo linasemekana kuwa na bangi na bastola.
Mwanasheria wa mahakama amesema kwamba hukumu iliyotolewa kwa Gucci Mane ni sahihi ukizingatia mtiririko wa matukio ya uvunjaji sheria yaliyofanywa na rapa huyo.
Mwanasheria wa Gucci Manne ameiomba mahakama kuizingatia miezi 11 ambayo rapa huyo amekuwa kizuizini tangu Septemba 14, 2013 baada ya kushutumiwa. Hata hivyo hakimu Jones alisema ombi hilo analiachia magerza itumie mamlaka yake.
Kifungo hicho cha Gucci Manne kimeambatanishwa na adhabu nyingine kama kutokuruhusiwa kusafiri wakati wote wa kifungo na kulipa faini ya dola za Marekani 5,000.