Diamond Platnumz alipata kashfa ya kuchelewa katika show jijini Stuttgart , Ujerumani, kitendo ambacho kilipelekea mashabiki kupaniki na kufanya vurugu katika ukumbi wa Melody Centre. Hata hivyo Diamond alijitetea na kuomba radhi akidai kuwa halikuwa kosa lake. Katika kusafisha taswira yake na taswira ya waandaaji wa tukio hilo Britts Events, mkali huyo wa Mdogomdogo atafanya show ya bure kabisa kama tangazo linavyoonesha katika picha.
Show hiyo itafanyika Septemba 20, 2014 katika ukumbi ule ule ambao mashabiki walileta vurugu.
Katika ukurasa wake wa Facebook Diamond amethibitisha hivi
Post by Diamond Platnumz.