Wanandoa ambao waliidhinishwa mnamo tarehe 30 Agosti wameendelea kubugia fungate katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu ikiwemo Tanzania. Mwandada Gabrielle Union ambaye ni muigizaji wa nchini Marekani pamoja na mumewe Dwayne Wade ambaye ni mcheza kikapu wa NBA jana walitimba rasmi Tanzania na kujiachia katika mbuga ya Serengeti. Tukio hilo lilibainika baada ya Gabrielle Union mwenye miaka 41 kupost picha kwenye mtandao wa instagram akiwa katika kiunga hicho cha Tanzania, yeye na Dwayne.
Pia walipata picha kadhaa na wenyeji wa maeneo hayo ambao ni wamasai.
Hii inadhihirisha kuwa Tanzania yetu ni nzuri hadi wageni wanaipenda. Na bata pia lipo la kutosha.