Khaleed Mohammed a.k.a TID amewashitua mashabiki wake baada ya kusema ana mpango wa kuhamia Kenya kufanya shughuli zake za muziki.
Amesema amefikia uamuzi huo kutokana na kazi zake nyingi kukubalika zaidi Kenya kuliko hapa nchini.
TID ambaye anatamba na kibao chake cha ‘Pressure’ alichoshirikiana na Nazizi alisema anaamini atapata mafanikio akiwa nchini humo.
“Nakubalika sana Kenya nafikiria kuhamia huko kimuziki kwa ajili ya kutafuta mafanikio, “alisema TID.