Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Mkambala a.k.a Jux, amemwagia sifa nyingi Vannesa Mdee a.k.a V. Money, akisema anamfaa afunge naye ndoa.
Amesema anaamini Vanessa anamfaa, japokuwa yamekuwepo maneno ya wawili hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Jux alimwambia Mwandishi Wetu kwamba kila mwanamke ana sifa yake yeye anavutiwa sana na V. Money.
Kutokana na kuvutiwa na kimwana huyo Jux angependa awe mkewe mambo yakiwa shwari.
“Napenda namna alivyo Vannesa hiyo inanifanya niwe naye karibu muda wote lakini kwa sasa ni rafiki yangu wa kawaida na hatuna uhusiano wa kimapenzi,” alisema Jux.