HABARI kutoka Nigeria zimesema mwigizaji maarufu wa kiume wa sinema nchini humo, Muna Obiekwe, amefariki jana katika hospitali ya Festac, jijini Lagos, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa figo.
Mojawapo ya filamu aliyocheza Muna.
Vyanzo vilivyokuwa karibu na mwigizaji huyo, vinasema Muna alikuwa akipambana na matatizo ya figo ambayo alikuwa ameyafanya siri kwa muda mrefu kabla ya kumwambia rais wa chama cha waigizaji cha Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima, ambaye aliendelea kuwa karibu naye.
Habari hizo zinasema kwamba tabia ya kutumia sana vileo ya mwigizaji huyo ambaye makazi yake yalikuwa katika mji wa Enugu, inaweza isihusiane na matatizo yaliyosababisha kifo chake.
Muna atakumbukwa katika baadhi ya filamu zake kama: He Lives in Me, Songs Of Sorrow, Enemies in Love, It’s Juliet or No One, Wasted Effort na zinginezo.
Msanii mwenzake kutoka Nollywood, Nonso Diobi, amethibitisha kifo hicho baada ya kuwepo sintofahamu kutoka kwa baadhi ya watu waliokuwa wakiweka taarifa katika mtandao wa Twitter kuwa Muna hajafariki.
Nonso amethibitisha kifo hicho baada ya kuwasiliana na rais wa chama cha waigizaji cha Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima na kuwataka watu waliokuwa wakipotosha kuhusu kifo hicho kuacha mara moja.
Zifuatazo ni baadhi ya meseji zilizokuwa zikitumwa katika mitandao ya kijamii kuanzia jana: