Baada ya story kuwa kubwa kuwa Wema Sepetu alimpeleka mpenzi wake
wa zamani Diamond Mahakamani gazeti hili leo limeomba radhi kutokana na
habari hiyo.
Nukuu;
“Katika gazeti letu la Mtanzania toleo No. 7709 la Alhamisi Januari
22, mwaka huu, tuliandika kimakosa stori yenye kichwa cha habari ‘Wema
Sepetu ampeleka Diamond Polisi’. Baada ya kufanya uchunguzi
tumejiridhisha habari ile haikuwa na ukweli, kwani chanzo kilichotupatia
kilitupotosha, hivyo kuleta usumbufu kwa msanii Wema pamoja na jamii.”
“Kutokana na hali hiyo, tunapenda kumwomba radhi Wema na familia
yake. Siku zote sisi MTANZANIA tumekuwa makini katika kusimamia misingi
ya habari za weledi na haki kwa jamii”.