Mbunifu wa mavazi wa
kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania
kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi
katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Rais
mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria Ngowi akila
kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika sherehe za zilizofanyika
jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Guy Scott, of Scottish
Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati
jeupe na tai nyekundu
zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu
aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani
hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
Akizungumza baada ya hafla
hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya
kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni
hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.
Rais
mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria Ngowi akitia
saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za
kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.
“Hii ni hatua kubwa katika
kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa
kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya
kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa
Edgar Lungu”, alisema Ngowi.
Mbunifu Ngowi alisisitiza
kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya
mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya
kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika
sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na
aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte,
Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi
mbalimbali pamoja na wananchi wake.
Rais
mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria Ngowi akiwa na Mkewe Eshter Lungu Muda mfupi baada ya
kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika
viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Mbunifu huyo ameendelea
kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza
kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta
mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu
kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka
Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho
ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes
Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.
Hii ni changamoto pia kwa
wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili
kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile
Sheria Ngowi alivyofungua mlango