Mwanamuziki maarufu nchini na sehemu nyingi za dunia – Diamond Platnumz ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mwanadada Wema Sepetu ameendelea kuuhakikishia ulimwengu kuwa, mpenzi wake wa sasa ZARI al-maarufu kama “The boss lady”, ni mama mtarajiwa aliyebeba ujauzito wa msanii huyo nguli nchini na kwamba hii sio project nyingine.
Huku akitumia mafumbo kwenye maneno yake ambayo wataalamu wetu wa Kiswahili ndio wametufafanulia kisanifu zaidi, Diamond aliandika
“Kileeeeeeee kinaanza kumuharibia mtu Mavazi..”
huku akiweka picha yake na mpenzi wake huyo wakitoka kwenye show ya miaka 38 ya CCM huko songea. Baada ya kukaa chini vizuri na wataalamu wetu hawa wa fasihi , walituhakikishia kuwa “Kileeeee” katika sentensi hiyo sio kitu kingine bali ni ujauzito alionao mrembo huyo na mara nyingi ukichunguza ndio kitu kinachomuharibia mwanadada au yoyote mavazi kirahisi hasa “kinapoanza” kuwa kikubwa.
Kweli tumeamini lazima ujue tofauti ya msalaba na kujumlisha.