Ule ugonjwa wa kuvuja kwa nyimbo za wasanii ambacho hazijakamilika au muda wake wa kutoka bado time hii imemkuta Ney wa Mitego baada ya wimbo wake mpya uitwao Only One kuenea kwenye mitandao mbalimbali.
Akiongea na millardayo.com alisema; “Mimi sijawahi kuvujiwa na wimbo kiukweli kabisa labda kitambo sana kipindi hicho nilikuwa sina nguvu kubwa yaani kujulikana, lakini kwa mara ya kwanza imenikuta juzi, ni wimbo wangu mpya Only One ambao niliimba kwa hisia zangu mwenyewe ukiangalia ni wimbo ambao upo kwenye maadhi ya R&B nikasema nahitaji kuimba wimbo wa mapenzi, sikuweka akili kabisa kama nitakuja kuutoa rasmi lakini mipango yangu ilikuwa kama nitakuja kuutoa kwenye albam yangu inshallah Mungu akijaalia…
Sasa nashangaa kuona wimbo umeshatoka bila ruksa yangu yaani upo tayari kwenye mitandao, nahisi utakuwa ni utaratibu wa studio ndio chanzo cha kuvuja kwa wimbo wangu….’alisema.
Hii ndio single ya Ney wa Mitego iliyovuja kwenye mitandao mbalimbali uusikilize #Onlyone bonyeza play hapa
MILLARD AYO