Video ya hit song ‘Mwana‘ ya Ali Kiba Feb 3 2015 imepitishwa na kuoneshwa kwenye kituo kikubwa cha TV cha Trace TV kilichopo Ufaransa ambacho Wasanii wengi wakubwa wa Afrika wamekua wakionyesha furaha yao pindi video zao zinapogongwa kwenye TV hii ambayo imebarikiwa kuwa na nguvu ya kipekee kwenye muziki wa kizazi hiki.
Video ya Mwana ni video nyingine ya Tanzania kwa mwaka 2015 kufanikiwa kuchezwa kama video mpya kwenye kituo hicho baada ya ‘Nitampata wapi‘ ya Diamond Platnumzkuingia kwenye chati yao ya Top 10 hivi karibuni.
CHANZO; MILLARD AYO