Msanii chipukizi Furaha Magaho a.k.a F Gao ameutendea haki wimbo uliovuja wa mkali Diamond Platnumz baada ya kuupamba kwa kiitikio na ubeti maridhawa. Wimbo huo unaokwenda kwa jina la Maradhi ya Moyo umesemekana kuvuja mwanzoni mwa mwezi Februari na baadae chipukizi huyo akaingiza chorus na verse moja.
Daktarii wangu ,, sweet ,. wangu sweet… ni chorus ambayo huwezi kuacha kuirudia rudia ukisikiliza wimbo huo. Nimeuweka hapa wimbo huo ili na masikio yako yaamue na mdomo ukiri kama hii remix ni tamu kama Mcharo au laa.