MSANII wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kumchukua mpenzi wa
msanii wa filamu ambaye pia ni mpigapicha, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’
aliyejulikana kwa jina moja la Vivian.
Chanzo cha habari kililiambia gazeti hili kuwa, tangu Wolper awe karibu
na Vivi, Farid amekuwa akiumia sana kwani amekuwa akikosa muda wa
kujiachia naye.
“Yaani Wolper kampora Farid Vivi wake, sasa hivi jamaa ameamua kumuacha maana anaona mambo hayaendi sawa.
“Watu wanajiuliza, Wolper anampa nini Vivi? Ni ushosti wa kawaida tu au
kuna kingine. Maana mtu huwezi kumuacha mpenzi wako kisa msichana
mwenzako,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Farid na
alipopatikana alisema ni kweli Vivi alikuwa mpenzi wake lakini Wolper
kampora.
“Vivian alikuwa ni mpenzi wangu lakini baada ya kuwa na urafiki na Wolper alibadilika na kunikataa.
Demu aliyoporwa |
“Nilishindwa kujua sababu ya yeye kutotaka kuwa na mimi kwa kuwa Wolper
ni msichana mwenzake. Inaniuma sana kwani nilikuwa nampenda sana, hata
hivyo siwezi kumrudia kwani atakuwa ameshaharibika kitabia,” alisema
Farid.
Alipotafutwa Wolper kuzungumzia madai hayo alisema, anashangazwa na
taarifa hizo na anachokijua yeye ni kwamba Vivian ni rafiki yake Farid
ni mtu wake.
Farid Uwezo |
“Kwanza Farid ni mtu wangu wa karibu sana ambaye sidhani kama anaweza
kusema maneno hayo. Pili Vivian ni rafiki yagu wa kawaida, mimi nadhani
kuna maadui zangu wanataka kunichafua,” alisema Wolper.
GPL