Imeripotiwa kuwa mmoja wa wapenzi wa msanii maarufu kutoka Nigeria Davido ni mjamzito.
Mwanamke huyo ambaye ametambulika kwa jina la Sophie Momodu amethibitisha kuwa na mimba ya msanii huyo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na mwandishi mmoja inasemekana
wawili hawa walikutana mwezi wa saba mwaka 2014 usiku jijini Abuja baada
ya Davido kumaliza kupiga show yake kwenye chuo kikuu cha jijini hapo
Uhusiano wa Davido na mrembo huyo ulikuwa maarufu mwanzoni wa mwezi
wa tisa mwaka jana ingawa kikundi cha msanii huyo akikuunga mkono
uhusiano huo kutokana na Sophie kutokuwa maarufu.