Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz anatarajia kuzindua televisheni yake kwenye Zari White Party itakayofanyika Ijumaa hii huko Mlimani City, Mwenge, jijini Dar.
Pamoja na vitu vingi vitakavyokuwepo siku hiyo mashabiki watashuhudia uzinduzi wa Tv hiyo kwa mara ya kwanza ambapo Diamond atataja rasmi jina la Tv hiyo.