Mwanadada Taylor Swift amepata baraka ya kuisambaratisha rekord aliyokuwa akishikilia Nick Minaj. Taylor Swift kupitia wimbo wake mpya wa Bad Blood aliomshirikisha rapa Kendrick Lamar ameweza kuwateka watazamaji milioni 20.1 ndani ya masaa 24 katika akaunti ya VEVO na kuifunika Anakonda ya Nick Minaj ambayo ilifikisha milioni 19.6 kwa masaa 24.
Nimeiweka hapa video ya Taylor Swift “Bad Blood” uweze kuitazama kama bado hujaiona:
Harakati360 inakuletea habari kama hizi kwa ajili ya kutii hitaji lako la taarifa.