Mkali ambaye yupo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Grammy, Chris Brown ameachia video ya wimbo ‘Autumn Leaves’ aliofanya na mkali wa mashairi Kendrick Lamar. Kinachovutia zaidi katika video hiyo iliyogubikwa na mandhari ya kieshia ni uwepo wa Karrueche Tran kama moja ya video vixen.
Breezy anaonekana kupigania penzi la mrembo wake huyo wa muda mrefu katika video huku akimuonesha mapenzi kwa kumkiss.
Rapa Kendrick Lamar hajaonekana kabisa katika video hiyo na badala yake Chris anaonekana akifuatisha verse ya Kendrick.
Nimeiweka hapa uweze kuishangaa kwa umakini zaidi mdau wangu wa maana: