Kabla ya mchezo wa fainali ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani, mwanamuziki nguli wa R&B Usher Raymond alikabidhiwa kipaza suti cha dhahabu na kupewa jukumu la kuimbisha wimbo wa taifa hilo.
Katika fainali hiyo iliyofanyika siku ya Alhamisi ikiwakutanisha Golden State Warriors na Cleveland Cavaliers, mkali huyo wa All Fall Down ambaye pia ni moja ya wamiliki wa Cleveland cavaliers aliugeuza kionjo cha wimbo huo na kuuimba katiaka mahadhi ya Soul.
Fainali hiyo ilimalizika kwa timu ya Golden State Warriors kuibuka kidedea kwa kuifunga Cleveland jumla ya vikapu 103-82. Tukio jingine kubwa katika mchezo huo ni la kinara wa NBA na Cavaliers kuumia baada ya kujigonga katika kamera akiwa amekwisha kufunga vikapu 20 katika fainali hiyo.