Ule usemi wa kiswahili usemao ‘zimwi likujualo halikuli likakwisha’ unazidi kuwa dhahiri pale mwanadada Amber Rose aliposhindwa kujizuia na kuweka wazi kuwa bado anamfikiria baba wa mtoto wake ambaye ni rapa Wiz Khalifa.
Amber Rose na Wiz Khalifa walijenga ghorofa ya huba ambayo hawakuishi kwa muda mrefu sana kwani walianza kuhusiana mwaka 2011, wakavishana pete ya uchumba mwaka 2012, na baada ya kumpata mtoto wao wa kiume aitwaye Sebastian Taylor mapema Februari 2013 wakaamua kufunga ndoa Julai 2013.
Ndoa ya wawili hao iliishi kw muda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa tu kwani Septemba 2014 wawili hao walitalikiana baada ya kutokea sintofahamu katika ndoa yao. Baada ya talaka Amber Rose ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa Kanye West walitifuana kwa maneno katika mitandao na mtaliki wake huyo kitu ambacho kilionyesha kuwa yeye na rapa wa ‘We Dem Boyz’ hawana mahusiano mazuri.
Leo Amber Rose ametema nyongo aliyoivumilia kwa muda mrefu baada ya kuweka wazi kuwa hawezi kujifariji kuwa anajisikia vizuri kuishi bila Khalifa. Rose ameandika kwa hisia nzito katika mtandao wa Instagram:
“Mwanaume ninayempenda siku zote, tulikwaruzana sehemu fulani, na hata kama hatutaruadiana tena (Ingawa ninasali, naota na kutumaini kuona tunarudiana) ataendelea kuwa mpenzi wa maisha yangu milele. Vyombo vya habari vinalifanya jambo hili kuonekana gumu lakini sivijali tunapaswa kuishi kiuhalisia na sio kama jamii inavyotaka. Tumeungana milele kwa sababu tulipata mtoto kupitia penzi letu. Kwa shida na raha tulizopitia katika mahusiano yetu bado moyo wangu hunidunda kila siku kwa sababu yake” Rose amezidi kulalama katika ujumbe alioacha katika picha hiyo ambayo anaonekana kumbusu khalifa katika picha “Naugua ninapojifariji kuwa ninafuraha bila yeye. Sina raha bila yeye. Yeye ndiye pekee anayeweza kunifanya niwe na furaha. Mbali na kitumbua cha maisha yetu kimeingia mchanga, bado yeye ndiye ataendelea kuumiliki moyo wangu”