Katika ujumbe wake wa kumpongeza AY kwenye siku yake ya kuzaliwa Jumapili hii, Diamond amedai kuwa AY ndiye aliyemuunganisha na Davido hadi wakafanya remix ya wimbo wake ‘Number One’ uliobadilisha maisha yake.
“Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na kutangaza kazi zetu kimataifa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pengine watu hawajui kuwa wewe ndio uliyeniwezeshea kufanikisha Collabo langu na Davido, Kuniunga na Godfather na vingi ambavyo naamini ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na daima nitahakikisha sikuangushiemoji…Happy birthday Bro.”
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, AY ameandika hivi :
July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa kuiona siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani. Mungu awalaze mahali pema peponi. Natamani mama yangu angekuwa hai aone jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na pengine afurahie jasho lake la kunizaa, kunilea na kunitunza.
Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha yangu, ni wengi siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya habari vyote kwa support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe shabiki yangu kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!