Imekuwa ni kawaida katika muziki Duniani kwa wasanii kuamua kufanya kazi pamoja hasa Mixtape na Album kitu ambacho kinaendelea mpaka sasa ambapo Lil Wayne na 2 Chainz wanaanda Mixtape ya pamoja inayoitwa ‘Colli Grove’.
Lil Wayne ambaye anatarajia kuachia Mixtape yake ya ‘No Ceiling 2’ November 26 mwaka huu ameungana na 2 Chainz ambaye pia anaandaa album yake mpya inayoitwa ‘B. C’ (Before Chainz) ambayo mpaka sasa imeshakamilika.
Aidha Lil Wayne na 2 Chainz sio wasanii wa kwanza kutoa kazi kwa kushirikiana kwani Drake na Future wameshafanya hivyo pamoja na Fetty Wap na French Montana.