Mahakama ya Mkoa wa Vuga, tarehe 13.03.2024 imemhukumu mshtakiwa Abrahman Abdallah Chande (23) wa Saateni Zanzibar kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia Silaha.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 10/09/2023 majira ya saa 02:00 usiku huko Saateni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ambapo aliiba simu aina ya Samsung yenye thamani ya shilingi 400,000 za Kitanzania pamoja na fedha taslimu 200,000 za Kitanzania mali ya mlalamikaji.
Mshtakiwa kabla ya kuiba fedha na simu alitumia nguvu kwa kumuwekea mlalamikaji panga shingoni jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu namba 280 cha sheria namba 6/2018, Sheria ya Zanzibar.
Akisoma maelezo ya hukumu, Hakimu Mheshimiwa Yahya Ussi Yahya amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi 7 wa upande wa mashtaka ambao hauna chembe ya shaka na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa mahakama ya Vuga tarehe 31.10.2023 na kupewa kesi namba 303/2023
#KonceptTvUpdates