Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro leo ameshuhudia zoezi la utiaji saini na Mkandarasi wa CHINA RAILWAY CONSTUCTION ENGINEERING GROUP (CRCEG) atakayejenga Uwanja mpya Jijini Arusha.
Ndumbaro amesema kwa sasa unajengwa uwanja wa kisasa kwa ajili ya AFCON 2027 wenye thamani ya Tsh Bilioni 286 na wenye uwezo wa kuchukua Mashabiki 30,000.
Wizara imependekeza uwanja huo utakuwa ukihusisha michezo mingine pia kama riadha na uitwe jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan Stadium kuweka heshima ya Rais wa awamu ya Sita wa Tanzania.
#KonceptTvUpdatesMuonekanowa uwanja utakavyokuwa baada ya kujengwa jijini Arusha