Akiba Commercial Bank (ACB) imeandaa hafla ya Futari kwa kuwaalika Wateja, Wafanyakazi pamoja na Wadau mbalimbali wa benki hiyo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 25 Machi, 2024 katika Hoteli ya Serena Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Bw. Silvest Arumasi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa sana.
Aidha, alisema kuwa, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono ndugu zetu Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake.
Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mwisho, Bw. Silvest Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja, amewaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.
Akiba Commercial Bank
Benki kwa maendeleo yako
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Akiba Commercial Bank Plc Bi. Catherine Kimaryo amewashukuru Wateja, Wafanyakazi na Wadau wote wa ACB kwa kuitikia kwa wingi mwaliko wa hafla ya futari uliofanyika Jumatatu tarehe 25 Machi, 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo . Pia hafla hiyo ilihudhuriwa na Sheikh wa Dar Es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar pamoja viongozi kadhaa wa Serikali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Catherine Kimaryo amesema kwamba Benki ya Akiba inatoa shukrani za dhati kwa wote walioweza kuhudhuria hafla hiyo kwa kuanzia kwa Mgeni rasmi na viongozi mbalimbali wa Serikali, Sheik wa Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi na wadau mbali mbali wa benki hiyo. .
Aidha, Bi. Kimaryo amewahakikishia wateja na wadau wote kuwa ACB itaendelea kutoa huduma kwa uweledi na ufanisi mkubwa ili kufikia matarajio yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameipongeza ACB kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024, akiongea katika hafla hiyo ambayo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi, Mhe. Mpogolo amesema kwamba “kitendo cha kufuturisha kilichofanywa na ACB ni ibada ambayo mwanadamu aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine na atapata thawabu kwa kufanya hivyo”.
Aidha, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.