Rais wa Marekani,Barack Obama amebambwa na mtandao wa kimbea zaidi duniani akicheza american football,akiwa ametupia kapelo,pensi na akiwa tumbo wazi pande za Visiwa vya Hawaii
Rais Obama alikua kwenye mapumziko ya siku 10 ya mwisho wa mwaka yeye na familia yake kwenye kambi ya Kaneohe Marine Corps Base na alionekana akidaka mpira na kujiachia kwenye michanga kama kawa na alirejea hivi karibuni nchini Marekani baada ya holiday na kuanza mishe mishe za kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 6,2012