LIVERPOOL imewaadhiri Arsenal
waliokuwa wanasifiwa wana ukuta mgumu, kwa kuwafumua mabao 5-1 katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa Anfiled.
Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na Skrtel dakika ya kwanza na 10, Sterling dakika ya 15 na 52 na Sturridge dakika ya 20.
Bao la kufutia machozi la Arsenal
lilifungwa na Arteta dakika ya 69 kwa penalti. Ushindi huo, unaifanya
Arsenal ibaki na pointi zake 55 katika nafasi ya pili baada ya kuchea
mechi 25, wakati Liverpool imefikisha pointi 50 baada ya mechi 25 pia,
ingawa inaendelea kubaki nafasi ya nne.
Huruma: Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere akiwa haamini macho yake juu ya kilichowakuta leo