Vitu vingine ni virahisi kuona vinatokea lakini ni vigumu kufanya na kufanikisha. Sehemu aliyofika Diamond kimafanikio katika Ulimwengu wa Muziki sio sehemu ya mchezo. Ni hivi majuzi tu tumeshuhudia akinyakua tuzo saba za KILI, pia yuko katika nafasi tatu za juu katika kuwania Tunzo za KORA, na zaidi amevunja rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kutajwa katika tunzo za MTV ila hii ya sasa imekuwa historia ya aina yake kwa mwanamuziki kutoka katika ardhi ya Tanzania kushiriki katika tunzo hizo kubwa nchini Marekani na Dunia kwa ujumla. Tunzo hizo huandaliwa na televisheni ya Black Entertainment Television kuanzia mwaka 2001.
Diamond ametajwa katika kipengele cha “BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA”, akiwa na wakali wengine kutoka Afrika kama Davido-Nigeria, Mafikizolo-South Africa, Tiwa Savage-Nigeria, Toofan na Sarkodie-Ghana. Sherehe ya utoaji wa tunzo itafanyika Juni 29 mwaka huu huko Los Angeles Marekani.
Katika kuonesha shukrani zake za dhati Diamond ameandika hivi katika ukurasa wake wa Twitter: