Real Madrid Alonso nje, Atletico Costa nje
Ni vita ya kihistoria ya magwiji wawili ambayo itapiganwa pale Lisbon kuanzia mishale ya saa 9.45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Real Madrid wakiwa na kombe la Copa De Reley Atletico Madrid wao ni mabingwa wa ligi kuu ya Hispania Laliga.
Mahasimu hao wa jiji la Madrid leo wanakipiga katika fainali kubwa zaidi Ulaya kwa ngazi ya klabu, UEFA Champions katika jiji la Lisbon Ureno. Madrid wao wamefika hatua ya fainali kwa kuwang’oa mabingwa watetezi Bayer Munich huku Atletico wametinga fainali kwa kuwatoa Chelsea katika hatua ya nusu fainali.
Jiji la Lisbon limefurika huku stori kubwa zikiwa ni nani atacheza na ni nani hatacheza, Atletico Madrid wataikosa huduma muhimu ya Diego Costa ambaye aliumia katika mchezo wa mwisho wa Laliga dhidi ya Barcelona katika mchezo ambao uliwapa ubingwa wa ligi kuu ya Hispania. Hata hivyo kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeoni ameonesha kutokuwa na wasiwasi kwa kuikosa huduma ya Costa.
Kwa upande wa Carlo Anceloti yeye wachezaji wake muhimu akiwemo Ronaldo ambaye aliumia katika mchezo wao wa mwisho wa Laliga. Xabi Alonso ni pengo kwa upande wa Real,huku hali ya Benzema na Pepe zikiwa hazieleweki.
Kutokuwepo kwa Costa ni faida kubwa kwa Real Madrid na kwa Ronaldo ambaye anapigania kiatu cha ufungaji bora wa ligi hiyo ya mabingwa.
Katka mechi zao za mwisho, Atletico walishinda mchezo wa ligi kuu pale Santiago Bernabeu kwa 1-0, kabla ya mchezo wa pili ambapo walitoka sare ya 2-2. Lakini katika michuano ya Copa De Reley, Real aliitoa Atletico kwa jumla ya mabao 5-0 katika hatua ya nusu fainali.
Kila shabiki anatetea upande wake, lakini wahenga wa soka huishia kusema mpira ni dakika 90.