Baada ya jana kufanya hafla ya maandalizi pale Versaile Ufaransa usiku huu ndio mpango mzima umekamilika pale Florence Italia
Ndani ya ukumbi wa Forte di Belvedere mjini Florence, Italia, rapper,producer na mwanamitindo Kanye West amefunga pingu za maisha na mwanadada mrembo na mwanamitindo pia. Fununu zilitawala anga la habari kwa muda mrefu juu ya muafaka wa wawilihao kuoana tangu waanze mahusiano yao ya kimapenzi na leo wameamua kuiambia Dunia kuwa hawaishi kisela tena bali kama mume na mke.
Harusi hiyo imehudhuriwa na wageni wasiopungua 200 huku rafiki wa karibu wa Kanye, Jay Z pamoja na Beyonce kutokuonekana katika sherehe hizo.
Mishemishe za maandalizi ya sherehe ya leo zilianza katika nchi ya Ufaransa katika jiji la Paris, na katika jiji ambalo jana jioni sherehe za maandalizi rasmi zilifanyika.
Kwa Kim hii ni ndoa ya tatu lakini kwa Kanye yeye ndo mara ya kwamza.
MWANAHARAKATI 360 inawatakia maisha marefu na yenye mafanikio zaidi.![Kim Kardashian and Kanye West (Photo by Marc Piasecki/GC Images)](http://blog.chron.com/celebritybuzz/files/2014/05/kanye-west-and-kim-kardashian-wed-in-florence.jpg)
![Kim Kardashian and Kanye West (Photo by Marc Piasecki/GC Images)](http://blog.chron.com/celebritybuzz/files/2014/05/kanye-west-and-kim-kardashian-wed-in-florence.jpg)