Usiku wa jana umemaliza ubishi uliotawala wiki kadhaa miongoni mwa mashabiki wa soka wa timu mbili za Madrid,HIspania.Ubishi umemalizika kule Lisbon na Real Madrid ndio mabingwa wa kombe la UEFA. Vijana wa Diego Simeon walishindwa kutunza bao walilopata dakika ya 36 kupitia kwa Gidgon, goi hilo lilisawzishwa dakika ya 93 na Sergio Ramos.
Hadi kumalizika kwa dakika 90 ubao wa magoli ulisomeka 1-1, ikambidi mwamuzi kuongeza dakika 30 kwa mujibu wa sheria ya soka, dakika ambazo zilishuhudia Gareth Bale, Marcelo na Ronaldo wakiipatia Real Madrid magoli matatu ambayo kwa ujumla yalifanya mchezo huo wa fainali kumaizika kwa Real kuipiga Atletico 4-1.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu hizo zikishambuliana kwa zamu.Kitu ambacho kiliibua sisimko katika mchezo huo ni pamoja na kuanza kwa mshambuliaji wa Atletico, Diego Costa ambaye mwanzoni alitajwa kutokuwepo katika kikosi. Costa alicheza dakika tisa za mwanzo kabla ya kuitwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Adrian Lopez.
Madrid wametimiza ndoto yao ya La Decima kwa kuchukua kikombe cha kumi cha michuano ya Ulaya huku ikiwa imelikosa kombe hilo kwa takribani miaka 12 tangu walipobeba ndoo ya UEFA kwa mara ya mwisho mwaka
Christiano Ronaldo naye ameendelea kuvunja rekodi kwa kufikisha magoli 17 katika michuano hiyo na kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika michuano hiyo, pia Ronaldo ameshinda kombe hilo la UEFA kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo msimu wa mwaka 2010.
Gareth Bale amedhihirisha kuwa mchezaji wa mechi kubwa baada ya kufunga goli la siku kama alivyoshinda pia katika fainali za Copa De Reley ingawa alikosa nafasi kadhaa ndani ya dakika 90.
Carlo Anceloti ameingia katika rekodi aliyokua akiishikilia meneja wa zamani wa Liverpool,Bob Paisley akiwa kocha pekee aliyeshinda vikombe vitatu vya Ulaya.
Kocha wa Atletico, Diego Simeon alipaniki katika dakika 30 za nyongeza na kuingia uwanjani mara mbili kitendo kilichomfanya mwamuzi amtoe katika benchi la ufundi sekunde chache kabla ya mchezo kumalizika.