|
Pharell Williums |
June 29 pale kwenye ukumbi wa Nokia Thearte jijini Los Angeles nchini Marekani, tutashuhudia tukio la ugawaji tunzo kwa washindi wa tunzo za BET Awards. Tunzo hizo ambazo huandaliwa na kituo cha redio cha BET kilichopo nchini humo kimewatangaza wasanii ambao watatoa burudani katika tukio hilo ambalo msanii kutoka katika ardhi ya Mwalinu Nyerere atahudhuria kwa mara ya kwanza akiwa mmoja ya wasanii wanaowania tunzo. Si mwingine bali ni Diamond Platnumz ambaye yupo kwenye kipengele cha Best International Act akiwakilisha Afrika pamoja na wakali wengine kama Davido wa Nigeria.
Kupitia mtandao wao wa BET wametoa orodha ya wasanii ambao watafanya shoo na hii ndo orodha yenyewe:
|
Jennifer Hudson |
|
Lionel Richie
|
|
Lil Wayne |
|
Trey Songz |
|
Usher Rymond
Msema Chochote au MC katika sherehe hiyo atakuwa Muigizaji nguli wa Marekani Chris Rock.
|