Mkali wa R&B na Pop kwa mbali, Justin Bieber amekuwa kimya kwa muda mrefu katka muziki. Katika maisha binafsi ameibuka na kubadilisha muonekano wake wa nywele kutoka nyeusi kwenda rangi ya platinum.
Lakini hiyo sio habari sana, habari ni yeye kuutambulisha mjengo wake ulioko huko Bervely Hills, California.
Jengo hilo ambalo sehemu kubwa ya kuta zake ni vioo lina ukubwa wa Futi za mraba 6,537 na parking yenye uwezo wa kuchukua magari 7.
Pia mjengo huo wa Bieber una vyumba sita vya kulala na mabafu 7.
E bwanaaee ni noma sana, ukilinganisha umri wa kinda huyo katika muziki na mafanikio yake.
Hizi hapa picha za mjengo wa Bieber