Moja ya mahusiano ambayo yamekuwa yakutokueleweka ni haya ya Chris Brown na Karueche.
Huwezi amini mkali huyo wa New Flame amemwagana tena na girlfriend wake wa muda mrefu na hii ameidhihirika usiku wa jana akiwa katika tamasha la Cali Chrismas ndani ya Power 106 huko Los Angeles baada ya kuwauliza mashabiki wa kike kama kuna ambaye yuko single. Chris alilifanya kitendo hicho wakati anapafomu Loyal na baada ya kimya kidogo alisema na yeye yuko single na kutoa maneno ya hasira kwa mpenzi wake.
Kuna wakati Chris Brown aliwahi kupost instagram ingawa alifuta post hiyo akidai kuwa Karrueche alimsaliti kwa kudate na hasimu wake Drake wakati alipokuwa jela.
Karrueche alionesha dalili hizo mwezi uliopita baada ya kutweet post inayoonesha kuwa yuko single tena.
Looks like I’m a single lady again 😏
— Karrueche Tran (@karrueche) November 26, 2014