Tiwa Savage halisi katika pozi. |
Mwanadada ambaye alijifanya kuwa mwanamuziki Tiwa Savage amekomkomba mwanasiasa wa chama cha Peoples Democratic Party (PDP) ambaye ni mgombea wa useneta katika jimbo la Lagos kiasi cha Naira 500,000. Kiasi hich cha fedha kilikuwa makubaliano ya mwanadada huyo kutumbuiza katika hafla ya chama cha PDP. Mgombea huyo aligundua kuwa mwanadada huyo hakuwa Tiwa Savage halisi baada ya kutokutokea katika hafla hiyo.
Mwanasiasa huyo anayefahamika kwa jina la Segun Adewale a.k.a Aeroland ameomba mashirika ya kifedha (benki) yamsaidie kuweza kufuatilia miamala ya Tiwa Savage fake ili muhalifu huyo aweze kubainika na ikibidi Aeroland apate kiwango chake cha fedha.