Wadau wa mwanamuziki Rihanna walihesabu mabati mwaka 2014 baada ya mkali huyo kumaliza mwaka bila kutoa wimbo mpya. Wikiendi hii Rihana ameanza mwaka kwa kukata kiu ya mashabiki wake baada ya kuachia ngoma kali, akimshirikisha mkongwe Paul MacCarteney pamoja na rapa Kanye West. Ngoma hiyo ambayo itakuwa kwenye albam yake ya kwanza tangu ahame Def Jam na kujiunga rasmi na Rock Nation inakwenda kwa jina la ‘FourFiveSeconds’.
Mwanadada Rihanna anonekana kujiandaa kutengeneza albam yake ya nane na project ndo imeanza kama hivyo. Nimetupia wimbo huo hapa upate kuusikiliza mdau wangu: